Sali na Papa

Njia ya Moyo

NJIA YA MOYO

Mitume wa Sala, ndivyo wanavyoitwa wengi wanaouishi utume huu, huutazama Moyo Mtakatifu wa Yesu kama ufunuo wa Upendo wa Mungu usio na mipaka. Kwa kutuhurumia sisi anaotupenda, Mungu alimtuma Mwanaye wa Pekee kuja ulimwenguni, kuwa pamoja nasi wadhambi japokuwa hakupenda wala kutenda dhambi. Alitupenda akatuhurumia hata kufa msalabani kwa ajili yetu. Akiwa duniani alitawatazama wote kwa huruma, akawasikiliza wote waliomjia kwa huruma, akawagusa na kuwabariki wengi kwa huruma... akawa Mchungaji Mwema mwenye kulihurumia kundi lake. Sisi mitume wake tunajitahidi kuwa macho, masikio, mikono... yake yenye huruma. Tunajifunza huruma kupitia Moyo wake. Tunatafakari huruma yake kwa ulimwengu, na kuifanya Utume wetu.

Sikiliza kwa Moyo

Tenga muda wa utulivu kwa sala na tafakari ili kutambua mwongozo wa Mungu katika maisha yako.

Tenda kwa Upendo

Geuza imani kuwa matendo kwa kumsaidia mwenye uhitaji na kujenga amani katika familia na jamii.

Endelea kwa Tumaini

Katika changamoto, shikilia matumaini na kumbuka kuwa safari ya kiroho hujengwa hatua kwa hatua.

Tafakari ya Leo

Moyo wenye upendo huanza kwa sala ndogo na tendo moja jema.