Sali na Papa
VIJANA WANA EKARISTIA (VWE/EYM) Tanzania

SISI NI NANI?.

Vijana Wana‑Ekaristia (Eucharistic Youth Movement, EYM) ni ushirika wa kimataifa kwa ajili ya malezi na maisha ya Kikristo ya watoto na vijana,

Mtandao wa VWE unawakaribisha vijana duniani kote kuishi kwa mfano wa Yesu, tena katika uhusiano na urafiki wa moyo kwa moyo na yeye. Mtindo wake wa maisha ni wa ki-Ekaristi kwa ajili ya utume wa Yesu duniani.

Nembo ya Njia ya Emau Msingi wake maisha ya VWE ni pedagogia (mbinu‑elimu) ya wanafunzi wa Emau: "Injili, Ekaristi, na Utume. Tunaweza basi kuiita hii “Njia ya Emau”"
Tulipotoka

HADITHI YETU VIJANA WANA EKARISTIA

Safari yetu inaendelea kuunganisha vijana na moyo wa Yesu katika kila kizazi.

1865

Mwanzo wetu

Hadithi yetu inaanza mwaka 1865 pale Papa Pius IX aliwapowaomba Wakatoliki wote waungane naye kwa sala na sadaka, kwa ajili ya amani ya dunia iliyokuwa pia ikihatarisha utume wa Kanisa. Akiwa amevutiwa na mwito huu, Padre Leonard Cross wa Ufaransa alipata wazo la kutumia hii kama fursa ya kuwaalika vijana kujiunga na utume huu muhimu. Hiyo ikawa ndiyo njiti ya kiberiti iliyowasha moto wa Vijana Wana Ekaristi.

Description
1881

Wazo Kusambaa kwa kasi ajabu

Wazo hili lilifanikiwa sana na likasambaa kwa kasi ajabu. Wakati wa Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Ekaristi mwaka 1881, tayari tulikuwa na wanachama 100,000 duniani kote! Mtakatifu Thérèse wa Lisieux (Mt. Teresa wa Mtoto Yesu) alikuwa kajiunga na utume huu tangu akiwa na umri wa miaka 12.

1914-1915

Msukumo Mpya Kutoka kwa Papa na Jina Jipya

Baba Mtakatifu Pius X alitupatia mwelekeo maalum, akiruhusu na kuhimiza watoto kupokea Komunyo hata wangali na miaka 7 katika barua yake ya kitume Quam Singulari. Pia alihimiza watoto kuiombea amani Ulaya iliyokuwa vitani. Hili lilipelekea Mkutano wa Kimataifa wa Ekaristi wa Lurdi mwaka 1914 kutoa mwito wa kuanzishwa muungano wa vikundi vya kiekaristi vya watoto. Mwaka mmoja baadaye, 1915, tukachukua jina “Kikosi cha Kiekaristi.” (Eucharistic Crusaders)

Description
1962

Mwanzo Mpya! Kuzaliwa kwa Mtandao wa Vijana ya Kiekaristi (VWE)

Hadithi yetu inachukua mwelekeo mpya na kusisimua mwaka 1962. Hapo ndipo tulipoanza kutumia rasmi jina tunalotumia leo: Mtandao ya Vijana Wana Ekaristia (Eucharistic Youth Movement, EYM). Hili haikuwa badiliko la jina tu, bali upyaisho kamili wa mtindo wetu wa malezi na maisha ya kiroho ili kuwafikia vijana kwa njia bora zaidi. Nguvu hii mpya ilisambaa haraka katika nchi nyingine nje ya Ulaya.

Description
Leo

Tawi rasmi la vijana, la Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni

Leo, Vijana Wana Ekaristia (VWE) ni tawi rasmi la vijana, la Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni (Pope’s Worldwide Prayer Network), na tupo katika nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Lengo letu kuu kwa maneno rahisi ni kuwasaidia vijana kujenga urafiki binafsi na Yesu, tukitumia Injili na Ekaristi kama mwongozo wetu. Sasa sisi ni kikundi cha pili kwa ukubwa cha vijana Wakatoliki duniani.

Description
Injili

KATIKA INJILI:

Tunafundishwa na Yesu juu ya Mapenzi ya Mungu.

Ekaristi

KATIKA EKARISTI:

Tunatambua mapendo ya Mungu katika Kristu yanayowekwa wazi kwetu kila siku.

Umisionari Mahalia

UMISIONARI MAHALIA:

Tukipewa mwelekeo na Injili na kupewa nguvu na Ekaristi, tunakuwa Mitume wa Yesu katika maisha yetu ya kawaida, pamoja na Kanisa la Yesu.

Hakuna Posti Mpya Kwa sasa, Tafadhali Rudi Baadae