Sali na Papa
icon

Sali na Papa - Asubuhi

Loading...

icon

Sali na Papa - Mchana

Loading...

icon

Sali na Papa - Jioni

Loading...

SALA YA MAJITOLEO YA KILA SIKU

SALA YA MAJITOLEO YA KILA SIKU

MAJITOLEO YA KILA SIKU

Ee Baba mwema,
natambua uko hapa pamoja nami.
Nakuja mbele yako katika siku hii mpya.
Weka moyo wangu kwa mara nyingine tena karibu na Moyo wa Mwanao Yesu,
anayejitoa kwa ajili yangu na anayekuja kwangu katika Ekaristi.
Roho wako Mtakatifu anifanye kuwa rafiki na mtume wake,
aliye tayari kwa utume wake wa huruma ulimwenguni.
Ninaweka mikononi mwako furaha na matumaini yangu,
kazi zangu na maumivu yangu,
mimi mzima na kila kitu nilichonacho,
kwa kushirikiana na kaka na dada zangu
wa Mtandao huu wa Sala Ulimwenguni.
Pamoja na Mama Maria,
ninakutolea siku yangu kwa ajili ya utume wa Kanisa
na kwa nia ya Sala ya Baba Mtakatifu [na Askofu wangu] kwa mwezi huu.
Amina

Tazama Video Mpya Za Papa Mtakatifu

Furahia video mpya kabisa kutoka kwa Papa Mtakatifu Kila Mwezi. Tembelea tovuti rasmi ya Papa Mtakatifu kwa video zaidi na habari zaidi.

SEPTEMBA | Kwa ajili ya utunzaji wa maji.

Tusali kwa ajili ya usimamizi endelevu na wa haki wa maji iliyo rasilimali muhimu, ili kila mtu awe na nafasi sawa ya kupata maji. The post SEPTEMBA | Kwa ajili ya utunzaji wa maji...

Video iliyotolewa: 1 September 2026

Angalia Video

Video ya hivi karibuni kutoka kwa tovuti ya Papa Mtakatifu.

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni ulianza mwaka 1844 huko Vals, Ufaransa, wakati Padre Francis Xavier Gautrelet SJ alipowahimiza vijana Wajesuiti (Wajezuiti Walelewa) kuwa mitume na wamisionari hata wawapo masomoni. Vijana hawa walianza kuyafanya majukumu yao ya kawaida kuwa matoleo ya kiroho. Mazoezi haya hapo awali yalijulikana kama Utume wa Sala (Apostleship of Prayer), yakaonesha umuhimu wa kuishi maisha ya utayari wa kitume wa kudumu; na kuongeza thamani ya kiroho ya shughuli za kawaida kwa “kuziunganisha na Sadaka Takatifu ya Kristu” kupitia Ibada Takatifu ya Misa. Kwa njia ya majitoleo binafsi ya kila siku, kila siku utayari huu wa kitume ulipyaishwa Utume huu ulienea haraka hata nje ya nyumba za Wajesuiti.

Jua Zaidi
about-image

Habari na Sala za Karibuni

Endelea kufuatilia ujumbe wetu mpya na waraka wa sala wa mwezi.

Sali Nasi
Waraka wa Sala, Mwezi Septemba
21 Sep 2026

Waraka wa Sala, Mwezi Septemba

Mwezi huu baba mtakatifu ana tusii tusali kwa ajili ya Huduma ya maji Ulimwenguni.

Soma Waraka wa Sala
HABARI

Habari Mpya

Tazama zote

Hakuna habari iliyochapishwa kwa sasa.

Mapartna & Washiriki

Tovuti na jumuiya tunazoshirikiana nazo katika kueneza sala, habari na ujumbe wa Injili.

Latest EYM Post

Tunakuonyesha chapisho jipya kabisa kutoka kwa EYM.

Hakuna chapisho la EYM hadi sasa. Tafadhali angalia tena baadaye.

Jiunge Nasi

kuwa sehemu ya Imani na Matumaini Ulimwenguni.